Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Makalla amesema utekelezaji wa Ilani na maendeleo yaliyofanywa na serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni turufu kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu
Akizungumza na wananchi katika eneo la Himo, wilaya ya Moshi vijijini, mkoani Kilimanjaro Juni 10.2025 akiwa katika ziara ya yake ya kujenga chama Makalla alieleza hayo akisisitiza kuwa Rais Dkt. Samia amepeleka maendeleo kwa wingi na kuwafanya kutotumia nguvu kuyaeleza pale muda utakapofika
Makalla amesema CCM inamuona Rais Dkt. Samia ni karata muhimu sana katika uchaguzi huo kwani kwa kazi alizozifanya anaingia katika historia kuwa kiongozi aliyoongoza kwa kupeleka fedha za maendeleo zinazoacha alama ambazo zitakipa nguvu chama chao hapo baadaye
Amesema Rais Dkt. Samia ametekeleza mambo mengi kwa kugusa sekta tofauti ikiwemo maji, umeme, elimu, afya, miundombinu ya barabara na mengineyo aambayo yamefilisi ajenda za wapinzani
Pia, Makalla amepongeza taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Vunjo Dkt. Charles Kimei kwani ameenda kata kwa kata na kueleza hali halisi ya miradi na kuainisha kwa uwazi pale palipokuwa na changamoto
Amesema baada ya kueleza mafanikio CCM ina wajibu wa kutatua changamoto na kukiri kupokea changamoto ya fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa kituo katika eneo la Gona na kuahidi kulifikisha kwa Waziri wa Ujenzi Abdallad Ulega kwa ajili ya kufanya tathmini ili waweze kupata stahiki zao.
