Last updated Apr 16, 2025

Mkurugenzi wa Radio E-FM na TVE, Francis Shiza ‘DJ Majizo’, leo Aprili 16, 2025 kupitia ukurasa wake wa Instagram, amempongeza mke wake, staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, kwa kutimiza mwaka mwingine wa maisha.

Katika ujumbe wake uliojaa mapenzi na shukrani, Majizo aliandika:
“Mke wangu, siku nne zilizopita nilichungulia ukurasa wako nikaona kuwa dua yako kubwa kwa Mungu ni kwamba ubarikiwe na uwe baraka.
Labda si kwa viwango unavyovitamani wewe, lakini Mungu ameshaijibu hiyo dua yako.
Umebarikiwa mengi, na wewe ni baraka kwangu, kwa watoto wetu, kwa wazazi wetu na kwa kila anayezunguka maisha yetu.
Namshukuru Mungu kwa kunibariki kwa kukupa wewe.”
Majizo hakusita kuonyesha furaha yake kwa siku hiyo maalum, akiongeza kwa ucheshi:
“Kwa hiyo umeongeza namba? Ongeza sauti ya spika yako ya Jizo, tuweke wimbo wa Happy Birthday!
Leo kaka atakuwa DJ, dada G ataimba, mimi na familia nzima tutakuwa dancers
Happy Birthday mke wangu!”
Ujumbe huo umegusa mioyo ya wengi mitandaoni, ukiwa ni ushuhuda wa ndoa yao yenye upendo na heshima.
