
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na kufanya mazungumza na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu ya Zanzibar ambapo pamoja na mambo mengine yalikuwa na lengo la kumwaga.
Katika mazungumzo yao Rais Mwinyi amemshukuru Jenerali Mabeyo kwa ushirikiano aliompatia wakati wakifanya kazi pamoja katika Wizara ya Ulinzi lakini pia amempongeza kwa utendaji kazi wake wa kulitumikia Taifa lake la Tanzania kwa juhudi na uadilifu wa hali ya juu.
Jenerali Mabeyo yupo katika ziara maalum ya kuaga wakati akijiandaa kustaafu.
Rais Mwinyi alifanya kazi na Jenerali Mabeyo kwa kipindi kirefu wakati akiwa Waziri Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Aidha, Dk. Mwinyi amemtakia kheri na maisha marefu Jenerali Mabeyo katika maisha yake mapya baada ya kustaafu.

