Hatma ya kugombea urais kwa Luhaga Mpina kupitia Chama cha ACT Wazalendo sasa imebaki mikononi mwa majaji watatu wa Mahakama Kuu Dodoma na itasikilizwa kwa siku tatu zijazo baada ya kesi hiyo kupangwa kusikiliza Septemba 11, mwaka huu.
Leo Jumatatu Septemba 8,2025 katika Mahakama Kuu hiyo ya Masijala Kuu Dodoma, Mpina na mgombea mwenza wake Fatuma Fereji wameshiriki kesi hiyo iliyokuwa mbele ya jopo la majaji watatu, Abdi Kagomba, Evaristo Longopa na John Kahyoza na mawakili watatu kutoka kila upande.
Mpina alienguliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya taarifa ya msajili wa vyama vya siasa kuzusha gumzo kutokana na katibu mwenezi wa ACT Wazalendo Monalisa kupiga Mpina kugombea Urais.
