
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai, amesema ulaji lishe duni unachangia kwa kiasi kikubwa upungufu nguvu za kiume.
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 23, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumzia tatizo hilo na kutoa mwito kwa waathiriwa kutokata tamaa bali waende katika kituo chake cha kutolea huduma za afya Ukonga Mongolandege watapata suluhu.
Mandai amefafanua maana ya ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume kuwa ni hali ya mwanaume kushindwa kufanya au kukamilisha tendo la ndoa kwa ufasaha.
“Miaka ya hivi karibuni tatizo hili limeonekana kuongezeka kwa kasi miongoni mwa wanaume walio wengi, hususan vijana ambao hapo awali ilikuwa ni nadra kusikia wakilalamika kusumbuliwa na tatizo hili.
“Tatizo hili linaonekana kuwakabili wanaume wengi duniani na kusababisha athari nyingi, ikiwamo kuvunjika uhusiano miongoni mwa wapenzi au ndoa.
“Kimsingi tatizo hili linaweza kugawanywa katika makundi matatu, ambayo ni pamoja na umbile la mwanaume kutokuwa imara kiasi cha kupelekea kushindwa kufanya tendo la kujamiiana au umbile la mwanaume kutokuwa na uwezo wa kusimama wakati wa tendo la ndoa.
“Hali hiyo mara nyingi huwa ni matokeo ya tabia ya kujichua ‘masturbation’ kwa kipindi kirefu.
“Sababu nyingine ni suala la umri, ambapo wataalam wa afya wanasema kuwa kadri mwanaume anavyoingia katika umri mkubwa ndipo nguvu zake za kiume hupungua.
“Watu wanaozeeka wakikuambia hawana nguvu za kiume huwezi kushangaa, lakini utashangaa vijana wa leo ndiyo wanakuambia hawana nguvu za kiume.
Tatizo hili pia huweza kuchangiwa na dosari za kimaumbile, ambapo kuna baadhi ya watu huzaliwa na udhaifu huo wa nguvu za kiume na wengine hupatwa na tatizo hilo mara baada ya kuzaliwa.
“Ukosefu wa lishe bora nayo ni sababu ya tatizo hili, iwapo mwanaume atakuwa na historia ya kusumbuliwa na utapiamlo, huweza kuchangia madhara kadhaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa nguvu za kiume.
“Sababu za kimaisha nazo huweza kuwa chanzo cha tatizo, hii humaanisha aina ya kazi ambazo mhusika anafanya, hususan za kutumia nguvu nyingi au wale ambao kazi zao ni za kusafiri sana.
“Kuishi katika mazingira usiyokubaliana nayo pia huweza kuchangia tatizo hilo, inaweza kuwa ni mazingira ya baridi au joto sana, vyote kwa pamoja huweza kuwa na madhara katika kupunguza nguvu za kiume.
“Sababu nyingine ni ajali ambazo humwacha mtu na maumivu makali, msongo wa mawazo, ulevi uliokithiri, uchovu wa mwili, matumizi holela ya dawa bila kupata ushauri wa wataalam, magonjwa kama kisukari na kupooza mwili,” amesema mtaalam Mandai.
