
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, amewapongeza wahitimu wa mafunzo ya ufundi kwenye chuo cha ufundi APEC kilichoko Kivule, manispaa ya Ilala, na kuwataka wahitimu kutumia ujuzi walioupata kujiari.
Kumbilamoto ametoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya Pili ya chuo hicho, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki, ambapo mgeni rasmi alikuwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Wilfred Mutafungwa.
Aidha, amewapongeza viongozi na walimu wa chuo hicho kwa kazi nzuri ya kuendelea kutoa mafunzo ambayo yamekuwa msaada mkubwa wa kujiajiri vijana wa kata ya Kivule na meneo ya jirani wanaonufaika na elimu ya chuo hicho.
Naye SACP Mutafungwa amewataka wahitimu kuwa mabalozi kwa jamii katika kusimamia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali za barabarani zisizo za lazima.
