
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai amesema tatizo la harufu mbaya ukeni linaweza kutatuliwa kwa aina mbili za mimea ya mjafari na muomboa.
Amesema mimea hiyo ina uwezo mkubwa wa kukabiliana na tatizo hilo na kumwacha salama mgonjwa husika.
Mandai amesema hayo leo Alhamaisi Desemba 8, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza matatizo mbalimbali ya kina mama walio katika umri wa uzazi.
“Chukua majani ya mjafari na muomboa yachemshe kunywa kikombe cha chai asubuhi na jioni muda wa siku 15 hadi mwezi mmoja.
“Au kausha magome ya mimea hii, kisha yasage na tumia kijiko kimoja cha chai cha unga wake kwenye maji moto au uji usio mzito. Kunywa siku 15 hadi 30.
“Aidha, kama umebaini una tatizo hilo mwone mtaalamu akuelekeze namna bora ya kutumia mimea hii kwa matokeo bora ya afya yako,” amesema mtaalam Mandai. Kwa wote wenye tatizo tajwa au matatizo mengine mbalimbali ya kiafya amewataka kwenda katika kituo chake cha kutolea huduma za afya Ukonga Mongo la Ndege, jijini Dar es Salaam au wampigie simu kwa namba 0745900600 iwapo wanataka ufafanuzi wa jambo lolote linalohusu afya au namna ya kufika katika kituo hicho.
