
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai, (pichani juu) amesema kunywa glasi moja ya juisi ya majani ya ngano kila asubuhi kabla ya kula chochote ni tiba ya mwasho mwilini.
Ameyasema hayo leo Jumatatu Juni 6, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati akielezea tatizo la kuwashwa mwili linavyoathiri baadhi ya watu.
“Juisi ya majani ya ngano ina nguvu kubwa ya kupambana na mazingira yasiyofaa ya mwili ambao bakteria wanasababisha kuwashwa ngozi.
“Pia unaweza kupaka juisi hiyo sehemu inayowasha. Mara nyingi kuwashwa sehemu yoyote ya mwili inakuwa na sababu moja au nyingine. Au inaweza kuwa ni dalili ya ugonjwa mwingine unaohitaji uchunguzi.

“Ni vema fanya vipimo kabla ya kuanza tiba ya aina yoyote licha ya kuwa juisi hii mara nyingi haiwi na madhara kwa mtumiaji kama zilivyo dawa nyingi asili,” amesema Mandai.
Hata hivyo, Mtaalam Mandai ametoa mwito kwa yeyote anayehangaika kwa kuugua ugonjwa wa aina yoyote kwenda katika kituo chake cha kutolea huduma za afya Ukonga, Mongo la Ndege, Dar es Salaam, ambako wagonjwa wanasikilizwa na kupewa huduma stahiki kwa upendo.
