Chini ya saa 24 baada ya Joe Biden kutangaza kuwa anaachana na azma ya kugombea urais kwa muhula wa pili, sasa njia ya Makamu wa Rais Kamala Harris kupata uteuzi wa urais kupitia chama cha Democratic iko wazi.
Kupata uteuzi linaweza kuwa jambo rahisi. Changamoto kubwa zaidi – ni kumshinda mgombea mteule wa Republican, Donald Trump mwezi Novemba.
Kulingana na kura za maoni za hivi karibuni, Bi Harris yuko nyuma ya Trump kwa asilimia ndogo tu – kama ilivyokuwa kwa Biden kabla ya tangazo lake la kihistoria.
Wanasiasa wakubwa wa chama chake wanamuunga mkono Harris, kama vile Spika wa zamani wa Bunge, Nancy Pelosi – mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa.
Fursa ya makamu wa rais dhidi ya Trump, ni kuvutia wapiga kura wa msimamo wa kati katika majimbo yanayobadilika-badilika na kuongeza ushawishi katika ngome za Democratic.
BBC Swahili.
