Jaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, Hamidu Mwanga amegoma kujitoa kusikiliza kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kesi hiyo ya madai ya mwaka 2025 imefunguliwa na Said Issa Mohamed, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chadema, Zanzibar na wajumbe wa Bodi ya wadhamini wa Chadema kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu.
Walalamikiwa ni Bodi ya wadhamini waliosajiliwa na Katibu Mkuu wa chama hicho.
Jaji Mwanga ameisikiliza kesi hiyo tangu Aprili 17, 2025 ilipotajwa kwa mara ya kwanza na kuendelea nayo katika hatua tofautitofauti.
Walalamikaji hao walimwandikia barua hiyo ya kumtaka ajitoe katika kesi hiyo Juni 23, 20255, huku wakimlalamikiwa kuwa na upendeleo kwa upande wa walalamikaji na mgongano wa masilahi na kuwa na mgogoro naye, malalamiko ambayo Jaji Mwanga aliyasikiliza Julai 14, 2025.
Katika uamuzi wake alioutoa leo Jumatatu, Julai 28, 2025 Jaji Mwanga amezikataa sababu zote zilizotolewa na walalamikiwa akieleza kuwa hazina mashiko.
Jaji Mwanga amesema sababu za walalamikiwa hao kumtaka ajitoe ziliegemea katika uamuzi wake alioutoa Juni 23, 2025 katika shauri la maombi madogo ya zuio la muda ya walalamikaji.Edited · (Picha kwa hisani wa Wasafi Media)
