Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Ziwa, Ezekiel Wenje, ametangaza rasmi kujiunga na CCM muda huu katika mkutano wa kampeni wa Dkt. Samia Suluhu Hassan unaofanyika Chato, mkoani Geita.
Wenje alikaribishwa ndani ya chama hichona mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni mgombea urais, Dk Samia Suluhu Hassani aliyeambatana na Katibu Mkuu Asharose Migiro.
