
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa Bodi mbalimbali huku akimteua Hawa Abdulrahman Ghasia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko Kariakoo na Sosthenes Kewe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Tanzania (TIB). Awali alikuwa Mshauri Binafsi wa Uendelezaji wa Sekta Binafsi za Fedha, Dar es Salaam.
Mhandisi Othman Sharif Khatib ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akichukua nafasi Dkt. Jones Kilembe ambaye Uteuzi wake umetenguliwa.
Dkt. David Nkanda Manyanza ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI)
Sylvester Jospeh Kainda ameteuliwa kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.

