
Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima, ameitika wito wa kufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, mjini Dodoma.
Gwajima ambaye pia ni Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, amewasili Viwanja vya Bunge leo Agosti 23, 2021 saa 6:40 mchana.
Anatakiwa kujibu tuhuma mbalimbali ikiwamo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya bunge.
Amefika mbele ya kamati hiyo baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kumtaka mbunge huyo pamoja na Mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa, kuhojiwa na kamati.
