Fahamu viwanja vitakavyochezwa mashindano ya CHAN
Nchi 19 zinajiandaa kuchuana katika mechi zitakazochezwa Nairobi, Dar es Salaam, Kampala na Unguja. Jumla ya michezo 44 imepangwa kuanza na mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Tanzania dhidi ya Burkina Faso jijini Dar es Salaam.
Viwanja vitakavyotumika na uwezo wao wa kuingiza watu wangapi, Tanzania Kenya na Uganda na Unguja ni kama ifuatavyo:
Uwanja wa Kasarani, Nairobi – mashabiki 60,000, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam – mashabiki 60,000, Uwanja wa Taifa Mandela, Kampala – mashabiki 45,000, Uwanja wa Taifa wa Nyayo, Nairobi – mashabiki 30,000, Uwanja wa Amaan, Zanzibar – mashabiki 15,000.
Katika droo iliyofanyika Januari 15, 2025 jijini Nairobi, Kenya ilipangwa Kundi A lenye timu ya Morocco na DR Congo, Angola na Zambia.
Tanzania ipo Kundi B pamoja na Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Uganda katika Kundi C ikichuana na Niger, Guinea, Afrika Kusini na Algeria.
Wawakilishi wengine kutoka Kanda ya CECAFA ni Sudan ambao watacheza katika Kundi D pamoja na mabingwa watetezi Senegal, Nigeria na Equatorial Guinea.
