Mzigo huu si mdogo kwa umri wako, mzigo huu ni mkubwa. Kwa umri wako vishawishi ni vingi vya marafiki, ndugu na jamaa. Nafasi yako ile haina ndugu, haina rafiki, haina jamaa; ni nafasi ya kulitumikia taifa hili,” alisema Rais Samia.
Aidha, alimtaka Waziri Mkuu mpya kuhakikisha anaweka mbele maslahi ya wananchi na kusimamia kwa uadilifu majukumu yote aliyokabidhiwa.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba miongozo ya utendaji kazi mara baada ya kumuapisha kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uapisho wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck