
Mamlaka za mji wa Beni ulioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jana Jumapili zimetangaza amri ya kutotoka nje baada ya milipuko miwili ya mabomu kutoka katika siku moja.
Meya wa jiji hilo, Kanali Narcisse Muteba, alimesema hataki kuona mtu yeyote mtaani kwa kuwa zipo taarifa kuhusu mipango ya mashambulizi zaidi.
Katika tukio la hivi karibuni mtu aliyekuwa amebeba bomu alikufa wakati lilipolipuka nje ya kilabu moja ya pombe.
Mapema jana Jumapili takribani watu wawili walijeruhiwa wakati bomu lilipolipuka ndani ya Kanisa Katoliki katika mji huo huo.
Ilitokea muda mfupi kabla ya sherehe ya kipaimara cha watoto kuanza.
Ingawa haijulikani bado ni nani aliyehusika na milipuko hiyo, kikundi cha waasi waADF – hufanya mashambulio ya mara kwa mara katika mkoa huo na imeyalenga makanisa hapo awali. Mnamo Mei, maimamu wawili wanaojulikana kwa kuwakosoa waasi wa ADF walipigwa risasi na kuuawa – mmoja wao ndani ya msikiti.
