
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amemuelekeza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla kusimamia zuio la bodaboda na bajaji kuingia katikati ya jiji hilo.
Hatua hiyo inachukuliwa na Waziri Bashungwa baada uamuzi wa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kupiga marufuku bodaboda na bajaji kuingia mjini isipokuwa maeneo yaliyoainishwa.
Tangazo la kusitisha vyombo hivyo vya usafiri kuingia katikati ya jiji lilitolewa jana Jumatano Aprili 20, 2022.
“Bila shaka nia ni njema, ila dosari ipo kwenye kushughulikia jambo lenyewe. Serikali yetu ya Awamu ya Sita inatambua na kuthamini ajira za vijana wetu za bodaboda na bajaji kuwa ni ajira rasmi na wanajipatia riziki na familia zao.
“Namuelekeza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, kusimamia usitishwaji wa zuio hilo ili kutoa nafasi ya kufanya tafakuri zaidi,” amesema.
