Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi Jumuiya ya chama cha mapindizi CCM Taifa Ally Hapi (MNEC) amewataka viongozi wa jumuiya ya wazazi na viongozi wa chama hicho kuhamasisha wananchi wenye sifa ya kuwa viongozi bora wagombee nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa ili wasaidie katika kupeleka mbele maendeleo ya wananchi kwenye maeneo yao
Hapi alisema hayo wakati akizungumza na wananchi na wanachama wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Pwani baada ya kuwasili kwa ziara ya siku nne inayolenga kuimarisha jumuiya ya wazazi na kuimarisha chama cha Mapinduzi CCM ambapo alisema jumuiya za chama ni sehemu katika kuhakikisha chama kinashuka kwa wananchi waendelee kukiamini na kukipa ushindi kwenye chaguzi zote zijazo na kukifanya kiendelee kushika dola.
