
Mtaalam wa Virutubisho Tiba, Abdallah Mandai, amefichua nguvu ya kitiba iliyomo katika embe. Mandai amesema embe bichi ni tiba anuai ya maradhi ya kuhara.
Ametoa kauli hiyo leo Desemba 27, 2021, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumzia umuhimu wa kupanda aina mbalimbali za matunda kuzunguka makazi ya watu.

“Menya embe bichi, likate vipande na kuviweka katika chombo, changanya na unga wa pilipili manga pamoja na asali, kisha tafuna vipande hivyo vyenye mchanganyiko huo.
“Mchanganyiko wako utategemea kiwango cha vipande vya embe lako. Hata hivyo, usile zaidi ya embe mbili kwa kutwa moja. Endelea na tiba hii muda wa siku tatu, ” amesema Mtaalam Mandai.
Kuharisha ni kitendo cha kujisaidia kinyesi chenye majimaji mara kwa mara.
Mtaalamu huyo amesema hali hiyo hutokea baada ya utumbo mdogo kuwa na maji mengi ambayo yanashindwa kutoka mwiilini kwa njia za kawaida kama ya mkojo na jasho hivyo kutelemka kwenye utumbo mkubwa usio na uwezo wa kutunza maji.
