
Jeshi la Marekani limesema linabeba dhamana kwa kuwaua bila kukusudia raia 23 na kuwajeruhi wengine 10 katika maeneo ya vita mwaka uliopita.
Kwa mujibu wa ripoti ya wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon, idadi hiyo inajumuisha vifo vya raia katika operesheni zake nchini Afghanistan, Somalia, Yemen na Nigeria.
Ripoti hiyo inasema raia 10 walijeruhiwa katika harakati za kijeshi za Marekani.
Waathiriwa wengi ni raia wa Afghanistan ambako Pentagon inasema 20 waliuliwa.
Taarifa hiyo pia inasema raia mmoja aliuawa nchini Somalia Februari 2020 na mwingine nchini Iraq mwezi Machi.
Taarifa hiyo iliyochapishwa kwa umma haitaji ni wapi raia 23 alikouliwa. Ripoti hiyo inasema ingawa Bunge la Marekani lilitenga dola milioni tatu kwa Pentagon kuzilipa fidia familia za waathiriwa, hakuna fidia iliyolipwa.
