Shughuli za kila siku zimekuwa ni sababu ya mafanikio huku wakati mwingine zikichangia pia changamoto mbalimbali za maisha kama vile kuumia kazini na kuchoka sana.
Hakuna kazi ambayo unaweza kusema ndiyo husababisha ajali, bali kama wasemavyo waswahili ‘ajali haina kinga’, mtu anaweza kuumia wakati anafanya kazi yoyote iwe ya ofisini, nyumbani au shambani. Licha ya kuwa wakati mwingine kazi za viwandani zinamweka mfanyakazi katika uwezekano wa kupata majeraha pengine kuliko kazi nyingine kutokana na mazingira yake.
Baada ya mtu kupata jeraha kinachoangaliwa ni tiba atakayopata ili kumpa nafuu na hata kupona haraka. Hata hivyo, muda wa tiba ya kidonda unategemea ukubwa wake, na dawa za awali alizotumia baada ya kupata jeraha husika.
Kama umeumia sehemu yoyote ni vema ukatumia utomvu wa papai. Dawa hii ina maajabu makubwa katika kuponya kidonda au jeraha.

Namna ya kutumia:
~Changanya utomvu huo na mafuta ya ng’ombe, paka kwenye kidonda asubuhi na jioni.
~Hata kama mgonjwa ana kidonda ndugu, dawa hii inaweza kumsaidia pia.
Tunajali mgonjwa wa aina yoyote, tunatumia tiba lishe na virutubisho asili kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya zinazomsumbua binadamu.
Tiba Nyingine
Katika kurasa nyingine tumejadili magonjwa mbalimbali ikiwemo Kwikwi, pumu, vidonda vya tumbo, tatizo la nyonga na tatizo la Koo na mengineyo mengi.
Ndugu msomaji, uwe huru kuuliza maswali au kutoa maoni yako kuhusu makala hii. Na ikiwa una changamoto yoyote mpigie Mtaalam Abdallah Mandai kwa namba 0745 900600 na hakika utajibiwa kwa wakati muafaka.
