DR. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni katika bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika katika Shirika la Afya Duniani (WHO).
Dk Ndugulile, mtaalam wa afya ya umma alikuwa mmoja wa wagombea watano waliojitokeza kurithi mikoba ya Dk Matshidiso Moeti.
Dk Moeti, raia wa Botswana anatarajiwa kuhitimisha muhula wake wa pili kama Mkurugenzi wa Kanda wa WHO katika kikao cha 74 kinachoendelea cha Kamati ya Kanda ya Afrika ya WHO huko nchini Congo Brazzaville tangu Agosti 26 hadi Agosti 30, 2024.
Mtanzania huyo alikuwa akishindana na Dk Boureima Hama Sambo wa Niger, Dkt Richard Mihigo wa Rwanda, Dk N’da Konan Michel Ya wa Ivory Coast na Dkt Ibrahima Socé Fall wa Senegal.
