
Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema hatua ya deni la Taifa kufikia trilioni 70, ipo siku nchi itapigwa mnada.
Ndugai ametoa kauli hiyo wakati akizungumzia tozo za miamala ya simu zilizopitishwa na Bunge akieleza zilipitishwa kwa lazima na hadi sasa kuna majengo ya madarasa na vituo vya afya vilivyojengwa kwa fedha hizo.
Spika huyo amesema tozo za miamala ya simu zilipitishwa ili nchi iweze kutekeleza miradi yenyewe, badala ya kutegemea mikopo ambayo imekuza deni la Taifa kufikia TZ trilioni 70.
Amesisitiza haiwezekani miaka 60 baada ya uhuru nchi bado iwe ya kutembeza bakuli.
Ameitaka Serikali kuangalia namna mpya ya kupata mapato akiongeza, “Kipi ni bora, sisi Tanzania ya miaka 60 tuendelee kukopa madeni makubwa makubwa au tubanane tufanye wenyewe hapa?” amehoji Ndugai.
