
Naibu Rais wa Kenya, Dakta William Ruto, ameonekana kusalimu amri baada ya kusema atamwachia Mwenyezi Mungu kumsaidia katika azma yake ya kuwania kiti cha urais wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani, vyombo vya habari vya nchi hiyo vimeripoti.
Kwa Mujibu wa Gazeti la The Star, Rais Uhuru Kenyatta amesema atamuunga mkono mmoja wa viongozi wa muungano wa upinzani wa Nasa kugombea nafasi hiyo.
Gazeti hilo linasema Rais alitoa kauli hiyo alipokutana na viongozi kutoka eneo la Mashariki mwa Kenya, katika Ikulu ya Nairobi.
Katika hatua ambayo inaonekana kujibu kauli ya Rais Kenyatta, Ruto aliandika katika mtandao wa Twitter jana Jumanne kuelezea hisia zake akiambatanisha na gazeti hilo.
