Mungu ametupa aina mbalimbali za mimea ili iwe msaada kwetu kwa mambo mengi likiwamo suala la tiba ya magonjwa mbalimbali yanayosumbua watu katika jamii.
Kama ilivyo njaa inapomkabili mwanadamu anapaswa kula chakula kwa wakati, ndivyo magonjwa nayo yanahitaji tiba ya mapema ili kukabiliana nayo.
Leo tutazungumzia faida za mtopetope. Na tutaangazia aina mbili za mmea huu yaani topetope pori na lile la kisasa ambapo tutaanza na topetope pori.
TOPETOPE PORI
Katika kujikinga na saratani za aina mbalimbali tumia majani ya mtopetope pori. Yatumie mara nyingi uwezavyo.
Namna ya kutumia;
~ Kausha kwenye kivuli majani ya mmea huu kisha yasage.
~Chukua unga wake tumia katika maji moto au uji usio mzito.
Hii ni kinga na tiba ya miongoni mwa aina mbalimbali za saratani iwapo zitagunduliwa mapema.
Mtopetope pori ambao unapatikana katika mikoa mingi hapa nchini, una saidia kupambana na maradhi.
Matunda ya topetope pori yana ganda laini na rangi njano inayovutia kuliwa.
Mti huo wa kiasili unaostawi sehemu zenye maji na kame, umeonesha uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi mengi na unasifika kwa kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya kalisi (calcium).
~Gome la mtopetope pori likipondwa na kubandikwa kwenye kidonda kibichi kinapona haraka mno, wazee wetu walilitumia pia kupoteza majipu hata yale makubwa yanayojulikana kama tambazi.
~Hali kadhalika gome la mtopetope pori likibandikwa katika uvimbe wa nje au kidonda na kwa uvimbe ulio ndani ya utumbo, mgonjwa anywe maji ya majani mabinchi ya mti huu baada ya kuyachemsha.
~Kutokana na mti huu kuwa kiboko ya vidonda vibichi, hata wale wanaotahiliwa kwa njia ya asili gome lake hutumika kuponyesha vidonda vya tohara.
~Mtopetope huu pia ni kinga ya maradhi mengi na una kiasi kikubwa cha protini na unaboresha mbegu za uzazi na hivyo kuongeza hisia zaidi za kufanya tendo la ndoa na kumuongezea nguvu mwanaume.
~Kwa kinamama wenye tatizo la kuziba mirija yao ya uzazi, wachemshe mizizi ya mmea huu na kisha kunywa maji yake, inasaidia kuondokana na tatizo hilo.
~Kijiko kimoja cha unga wa majani ya mti huu unaweza kuchanganya na maji moto, kunywa katika kikombe cha chai asubuhi, mchana na jioni ni kinga nzuri ya magonjwa mbalimbali.
Angalizo:
Ni vema ukanywa lishe tiba hii kabla ya kula.
Na hii ni sehemu ya kwanza ya tiba kwa kutumia topetope pori. Usikose kufuatilia makala zetu ili uweze kujifunza na sehemu ya pili ya tiba kwa kutumia topetope la kisasa.
Katika kurasa zetu kuna makala za magonjwa mbalimbali kama vile kwikwi, vidonda vya tumbo, miguu kuwaka moto, kisukari, bawasiri na magonjwa mengine mbalimbali.
Na ikiwa una changamoto yoyote katika masuala ya afya na matibabu kwa njia ya mimea tiba. Wasiliana na mtaalam Abdallah Mandai kupitia namba 0745 900600 na hakika utajibiwa kwa wakati muafaka.
